ALI BONGO:Atangazwa kuwa Rais na Mahakama ya Katiba ya Gabon.

Mahakama ya katiba nchini Gabon imethibitisha kuwa Ali Bongo ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 27 nchini humo.

Rais Bongo amepata 50,66% na mpinzani wake, mwenyekiti wa zamani wa Muungano wa Afrika Jean Ping 47,24%.

Matokeo ya awali yalionyesha ushindi wa Bongo kwa tofauti ndogo ya kura takriban 6000.

Kwa mujibu wa matokeo ya mwisho rasmi yaliotolewa na mahakama ya katiba Bongo alishinda na kura zaidi kutokana na kutobatilisha kura zilizopigwa katika ngome ya kiongozi huyo Haut-Ogoue.

Hatahivyo kura katika vitu 21 mjini Libreville zimefutiliwa mbali kutokana na ombi la upande wa kampeni ya rais. Na ndio sababu kiongozi huyo amepata asilimia kubwa zaidi katika matokeo ya mwisho.

Upinzani uliwasilisha malalamiko kupinga matokeo ya awali ya uchaguzi na kuiomba mahakama iamrishe kuhesabiwa upya kura hizo, katika eneo hilo la Haut-Ogoue, magharibi mwa Gabon ambapo rais Bongo ana wafuasi wengi.

Kumekuwa na wasiwasi katika mji mkuu Libreville kwamba huenda ghasia zikazuka baada ya mahakama ya katiba kutoa uamuzi wake.

Raia mmoja amenukuriwa na Shirika la utangazaji la UINGEREZA akisema: ” Nadhani kuna wasiwasi, watu wanataka kuwa salama, wanataka kununua vitu na kusubiria matokeo kwa makini nyumbani, iwao kila kitu kitakwenda sawa itakuwa vizuri”

Maduka mengi yameamua kufunga biashara kukwepa uporaji.Mapema mwezi huu huku biashara nyingi ziliathirika.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s