Jolie na Brad Pit wakanwa kweupee na MARION.

Marion Cotillard amevunja ukimya wake kuhusu talaka ya Brad Pitt na Angelina Jolie akikana kwamba alihusika kuvunja ndoa ya wawili hao.Msanii huyo wa Ufaransa alisema hayo katika chapisho lake la mtandao wa Instagram.

”Miaka mingi iliopita ,nilikutana na mpenzi wa maisha yangu.Yeye ndio penzi langu ,rafiki yangu na mtu ninayemuhitaji pekee”,alisema.

Cotillard pia alibaini kwamba yeye na mumewe Guillaume Canet walitarajia mtoto wao wa pili.

Maisha ya faragha ya msanii huyo mwenye umri wa miaka 40 yaliwekwa katika vyombo vya habari kufuatia habari kwamba Jolie alikuwa amewasilisha ombi la talaka kufuatia tofauti zisizotatulika.

”Hili ndio tamko langu la kwanza kuhusu habari za kuvunjika kwa ndoa hiyo,alisema.Sipendelea kuzungumzia kuhusu maswala kama haya ama hata kuyachukulia kwa uzito mkubwa lakini ninalazimika kufanya hivyo kwa sababu habari hizi zinawaathiri watu ninaowapenda”.

“kwanza miaka mingi iliopita nilikutana na maisha yangu,baba ya mtoto wangu wa kiume na mwana ninayetarajia,.Yeye ndio mpenzi wangu na rafiki yangu mkubwa,na mtu ninaye hitaji pekee”.

”Pili,wale wote wanaodhani mimi ni mkiwa ,sina tatizo lolote.Na kwa vyombo vyote vya habari na mahasimu wangu wanaopenda kuwahukumu wenzao kwa haraka ,ningependa Angelina Jolie na Brad Pitt ,watu ninaowaheshimu sana wawe na amani wakati huu mgumu”..

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s