#DonaldTrump Aomba msamaha kwa Kuwatukana Wanawake.

Mgombea urais wa chama cha Republican Marekani, Donald Trump, ameomba msamaha kwa matamshi machafu aliyotoa kuhusu wanawake katika kanda ya video iliyozuka ya miaka 11 iliopita.

Katika kanda hiyo, Trump anasikika akijigamba kuhusu kuwagusa wanawake sehemu zao za siri na kujaribi kushiriki ngono nao, anasema: ‘unaweza kufanya chochote unapokuwa nyota’.trumgMgombea Urais wa Marekani kupitia Tiketi ya  Chama cha Republican Bw. Donald Trump

Maafisa wakuu wa chama cha Republican wameshutumu vikali matamshi yake akiwemo spika wa bunge, Paul Ryan, aliyesema amechafuzwa roho na matamshi hayo.

Mhariri wa BBC wa eneo la Amerika kaskazini anasema hiki ni kiwango cha mzozo katika azma ya Trump kuwania urais wa Marekani

Katika kanda iliyorekodiwa Trump aliomba radhi kwa kuonekana akisoma , na ameahidi kuwa mwanamume bora zaidi lakini amemshutumu Bill Clinton kwa kuwanyanyasa wanawake kingono.

Amemshutumu Hillary Clinton pia kwa kuwakandamiza na kuwaibisha waathiriwa wa unyanyasaji uliotekelezwa na mumewe.

  CHANZO:BBC SWAHILI

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s