@FidQ “Gharama ya Video haisaidii kuifanya iwe nzuri ” cc @wakazi

Imekuwa kawaida sasa kwa wasanii wakubwa Nchini kutengeneza video za kazi zao nche ya nchi kiasi kwqamba huwekeza pesa nyingi sana na tumeona sasa matokeo chanya ya wasanii hao moja ikiwa ni kufanikiwa kupata VIEWERS wengi kwenye kazi zao,kuwa nominated kwenye TUZO kubwa hapa Afrika na pia kupata Endorsement kwenye makampuni makubwa Nchini.

Mbali na faida hizo ambazo wasanii wengi wanazipata ,wengi wao wamekuwa na Hulka ya kuzungumzia gharama wanazotumia katika kuandaa Video hizo lakini hii ni tofauti Kwa rapa kutoka Mwanza FID Q.

“Kuhusu kiasi nilichotumia siwezi kutaja ,mimi sio msanii wa kusema bajeti ya fedha niliyoitumia ,wasanii wa nje wanatoa video kali na hawajawahi kuzungumzia bajeti za video zao kwa kuwa haiwezi kuwa au kusaidia kuwa nzuri ,isipokuwa nini umefanya ndani yake ”

Amesema gharama ya video haisadii kuifanya video  iwe nzuri bali ni kujituma na kuweka nguvu kubwa ya kifikra kamwe hauwezi kufeli.fid-q                                                            Rapa FidQ

“Work it off ,imefanikiwa kuchukua tuzo ya ZIFF 2016 ya wimbo Bora wa Afrika Mashariki kwa sababu niliwekeza nguvu kubwa kifikra na pesa kiasi ,kwa hiyo naamini kwamba ukiwekeza nguvu ya kifikra sidhani kama utafeli”

Hata hivyo ameshauri wasanii kama hawana uwezo wa kuandaa video nje ya nchi watengenezee hapahapa bongo kwani panafaa pia

Fid Q alizungumza hayo yote wakati akiwa kwenye mzunguuko wa Tamasha kubwa la Burudani nchini FIESTA linaloandaliwa na CLOUDS MEDIA GROUP Ikiwa ni mara yake ya 13  Fid q anashiriki mfululizo .

Kwa Habari mbalimbali ni Follow hapa Twitter Instagramna kulike ukurasa wangu wa facebook

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s