Mfalme wa Morocco aahidi kujenga Uwanja wa Mpira na Msikiti mkubwa zaidi nchini #Tanzania.

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema ujio wa Mfalme wa Morocco nchini Tanzania ni fursa kubwa ya kibiashara na uwekezaji kwa Tanzania na Morocco ambapo Tanzania imesaini mikataba 21 ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.jpm-na-mfalmeRais wa Tanzania Dk.Magufuli kulia na Mfalme wa  Morocco Mohamed VI

Rais Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco Mohammed VI ambapo amesema Tanzania ni eneo zuri la uwekezaji pamoja na kuainisha mambo mbalimbali katika mazungumzo yao ikiwemo uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini, utakaosaidia kukuza pato la taifa.Akitaja baadhi ya makubaliano, Rais Magufuli amekuwa kuwa ni pamoja Mfalme Mohamed VI kuihakikishia nchi kuwa kutakuwa na ndege ya moja kwa moja kutoka Rabat Morocco hadi Dar es Salaam Tanzania, kutolewa kwa nafasi kwa askari wa Tanzania takribani 150 watakaokwenda kujifunza masuala ya ulinzi na usalama nchini Morocco.

Rais Dkt. John Magufuli amesema amemuomba Mfalme  huyo kuijengea Tanzania Msikiti Mkubwa Jijini Dar es salaam na uwanja mkubwa wa mpira mkoani Dodoma jambo ambalo amekubali.

“Nimemuomba Mfalme atujengee uwanja mkubwa wa mpira mkoani Dodoma na Msikiti mkubwa Jijini Dar es salaam jambo ambalo amekubali kitu ambacho kitazidi kuongeza uhusiano wetu kati ya nchi hizi mbili” Amesema Rais Magufuli.

                                                     Chanzo:Mtembezi.com

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s