Mamia waandamana kenya kupinga ufisadi uliokithiri nchini humo.

Mamia ya watu wamekusanyika eneo la Freedom Corner katika Uwanja wa Uhuru Park, katikati mwa jiji la Nairobi, kuandamana kulalamikia wanachosema ni ongezeko la visa vya ufisadi serikalini.Maandamano hayo yanafanyika siku chache baada ya gazeti moja kuchapisha habari zinazodai jumla ya dola 50 milioni za Marekani katika wizara ya afya zilitumiwa vibaya au zimeporwa.Serikali imekanusha madai hayo mpaka sasa ingawaje vyombo vya habari bado vinaripoti taarifa hiyo.

Wanaharakati walioandaa maandamano ya leo wanamtaka Rais Uhuru Kenyatta achukue hatua la sivyo ajiuzulu kwenye wadhifa wake wa urais.Polisi wametumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya waandamanaji hao leo mapema jijini Nairobi.

                                                           CHANZO:BBC SWAHILI

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s