Babu wa Miaka 107 asema unywaji pombe kali asubuhi ndiyo siri ya umri wake

Babu wa Miaka 107 asema unywaji pombe kali asubuhi ndiyo siri ya umri wake.

Mzee Mariano Rotelli huenda akawa ni moja ya watu wenye umri mkubwa zaidi kwenye Mji wa Coweta huko Georgia Nchini Marekani kama sio duniani kote,sio jambo geni kukutana na wazee wenye umri mkubwa kidogo hata hapa tanzania ila ishu ni maswali na majibu aliyotoa huyu Babu wakati akijibu maswali aliyoulizwa na waandishi wa habari wa Gazeti la The Newnan Times-Helerd la huko Georgia kwenye Birthday yake ya miaka 107.

581b0fdf762c6-image

Mzee Mariano Rotelli kushoto akiwa na maswahiba wake

Babu huyo anaeonekana mwenye furaha na sura iliyochangamka aliulizwa na muandishi wa habari aeleze nini siri ya umri wake? yeye alijibu kuwa siri ni kunywa kikombe kimoja cha kahawa na Whisky kila asubuhi hata kabla ya kwenda kazi.

Nimekuwa nikichanganya kahawa na whisky kila asubuhi kwa miaka 100 sasa,Nimewahi kwenda kwa daktari mara tatu tu katika kipindi chote.Mke wangu Yeye alifariki ,lakini mimi ningali hai.” Mzee Mariano alijibu swali aliloulizwa ,Ripoti za awali zinasema mke wake alifariki miongo kadhaa iliyopita .

Binti yake, Nancy Tyre alisema ingawaje Baba yake ana umri mkubwa lakini huwa hababaishwi na chochote na pengine hiyo pia imechangia kwa maisha yake marefu.kwani hufanya kazi zake nyumbani na kupumzika muda mwingi hivyo haitaji matunzo mengi kama ilicvyo kwa wazee wengi kama yeye. “Baba yangu ni shupavu hababaishwi na chochote kile kwani kile pengine nayo huenda ikawa ni sababu ya kuishi muda mrefu hadi leo kwani hata kazi ndogo ndogo hapa nyumbani hufanya mwenyewe ingawaje huwa tunamshauri apumzike“Alisema Nancy huku akitabasamu kidogo .

Mzee huyo pia sio mtu wa mchezo mchezo hakuacha kuwashauri waandishi wa habari waliokuwa wakimhoji na kusema “Mnatakiwa kunywa kiasi na kufanya kila siku iendayo kama siku ya mapumziko “aliongeza pia kwa kusema “Mimi huwa sichagui aina ya Whisky kwani nimekuwa nikiletewa aina chungu nzima za whisky nakunywa na kahawa na najiona bado ni kijana

Kumekuwa na wazee wengi ambao hueleza siri zao za maisha marefu hapa Duniani wengi wao wamekuwa wakidai vyakula vya asili ndiyo vimewafanya kufikisha umri mkubwa pamoja na madawa ya asili.Lakini wengine kweli hudiliki kusema pombe za asili kama Ikeba kwa wale ndugu zangu wa Gairo ndiyo sababu za hao kuishi miaka mingi.Lakini madaktari na wataalamu wa masuala ya afya Ulimwenguni  wanaonya kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako.

Chanzo:DIZZIMONLINE.COM

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s