Nuh Mziwanda anafunga ndoa Jumamosi hii?

Yaani unaambiwa usithubutu kukutwa na hawa jamaa wanaojiita Shilawadu kwani ni Wapambe mpaka kero,Leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds fm waliongea na jamaa aliyejitambulisha kama shuhuda tu aliyemuona Nuh Mziwanda maeneo ya Msasani Sheli kunako makazi ya wazazi wa Mchumba wake,na kudai alisikia sauti ya mzee akimtaka Nuh Mziwanda alipe mahali ya Shilingi milioni  1, na kudai ya kuwa jumamosi hii Nuh Mziwanda atafunga  ndoa na mchumba wake huyo mpya baada ya kubwagana na Shilole.

nuh-akiwa-na-mpenzi-wake-mpya-aitwae-nawal

Shuhuda huyo anaesikika kutoka eneo la Msasani Sheli alianza kumwaga uhondo huo kwa kusema  ”Nuh Alikuja usiku akiwa kwenye gari IST nyeupe na alikuwa na washkaji zake, alikuja kukutana na mzee mwenyewe, alikuja akakutana na naye akapangiwa mahari shilingi milioni lakini hawakuingia ndani waliongelea kwenye gari, mzee sio mtu wa mchezo mchezo.  Mimi eneo ambalo sio mbali sana”

Lakini hata hivyo Nuh Mziwanda alikiri ya kuwa alionana na Baba mkwe wake lakini kwa mazungumzo binafsi alikataa hafungi ndoa Jumamosi wala hakuna ishu za mahari ya Milioni moja “”mimi nilikuwa na mazungumzo tofauti na baba mkwe wangu nashindwa kuelewa wewe umejuaje kama mimi nimekwenda kuonana na baba Mkwe wangu, sikutaka mambo yawe hivi lakini nimeshindwa kuelewa umejuaje wewe?” alisikika Nuh Mziwanda akimuuliza Mtangazaji wa segment hiyo ya You Heard Soudy Brown.Unaweza ukasikiliza Segment nzima ya You Heard hapa.

CHANZO:DIZZIMONLINE.COM

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s