AT hautamsikia tena!aitupia lawama Menejimenti yake.

Msanii maarufu wa muziki wa mduara kutoka visiwani Zanzibar AT,Ameamua  kufunguka ya moyoni kuhusu ubovu wa Menejimenti yake kwa kushindwa kumsimamia vizuri kwani amekuwa akijitahidi kufanya kila aliwezalo ili aweze kufikia malengo yake kimuziki lakini Uongozi wake bado unashindwa kufanya majukumu yake.

Msanii huyo ambae wengi wanamjua kwa staili yake ya Mipasho na Michambo ametumia fursa hiyo ya kutoa hayo yote kuwaelezea mashabiki yake kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika kua amefanya kila awezalo ili kutoa ngoma kwa mwaka huu lakini bado Menejimenti yake imeshindwa kusimamia na kutoa ngoma zake.

Awali ya yote namshukuru mungu kwa kwa neema zake zote pia kwa kuzilinda kauli zangu ingawa nyengine ni sumu kwa wengine nachukua fursa hii kuongea na wa Tzwota na wana EA pia nawashukuru sana #Radio zote na Tv stations zote na blogs na magazeti na wadau mbalimbali kijana wenu nimekuwa nikifanya bidii kubwa kueka heshima na ramani ya muziki wetu halisi ila wengi hawakujua nini nahitaji umaarufu tu au tuzo maana nimeanza kupata tuzo ya kwanza BBC Kabla sijawa maarufu mwaka 2005 na 6 wimbo wa mimi na Pijei nyama ni nyama vitu hivi huja muda wowote ule bila ya kutumia force ya aina yoyote mimi ni msanii ambae naamini sisimamiwi na mtu but najua mengi na naona makubwa yaliyo mbali nawapenda wasanii wenzangu isipokuwa wale wenye kujiona bora kuliko wengine hii nchi yetu ilabado tuna kazi ya kufika pakubwa ijapokuwa inavibaji vikubwa sana.”AT aliendelea kuandika na kuanza kusema.

Kwa wale wanaonipenda ambao ni mashabiki zangu poleni kwa kukosa haki zenu za msingi kutoka kwangu naomba mnisamehe niwahakikishie kwa uwezo wa mungu mwakani huenda ikawa ni mwaka wa neema nyie.Hayo yote ni sababu naheshimu wakati na mipangilio ya kila hatua watu wa media tumeongea mengi sana leo yote yanakuja moja baada ya jingine niliwahi kusema msanii mzuri ni yule sie yule mwenye collaboration nyingi bali ni yule mwenye kufanya music mzuri na tofauti na wenziwe.“AT hakuishiwa maneno aliendelea kufunguka zaidi

Siku nikiwa na usimamizi mzuri ndiyo mtanielewa zaidi who iam i kwa sasa Nidharauni , nisemeni,nichekeni,nizibieni ila kunichamba tu ndiyo hamtaweza hata mchukue na india wote.uwezo wa kufanya collaboration na yoyote upo ila upande wangu wa Promotionhaupo OK kwahiyo haitaleta maana so niwaombe mashabiki wote rasmi nipo likizo hadi mwakani inshallah tegemea mabadiliko kuanzia Insta video hadi Audio nimekidhi haja ya kulipa deni upande wa shows nashukuru wote mmekuwa mkiona sijawaimbia juu ya CD (playback) hiko kipimo ndicho kipimo cha ukweli wa kipaji huru next up is Kazi yao.“Alimaliza kwa kusema hayo ya moyoni.

Kwasasa AT ametoa wimbo mmoja tu wa Kimbaumbau alioshirikiana na Peter Msechu lakini hata hivyo wimbo huo haujawa na rotation nzuri kwenye media.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s