Tundu Lissu aitwa Polisi kwa mahojiano juu ya sakata la Ben Saanane

Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Tundu Lissu ameitwa na Jeshi la polisi Dar es Salaam, kwaajili ya mahojiano kuhusu taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari hivi karibuni kuhusu Ben Saanane ambaye ni msaidizi wa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Image result for tundu lissu

 

Wakili Peter Kibatala ambaye ni Mkurugenzi wa idara ya sheria Chadema, amelithibitishia Gazeti la MWANANCHI kuhusu kuitwa kwa Lissu na kuhojiwa na polisi.

“Ni kweli ameitwa na polisi na yupo central mpaka sasa. Aliitwa tangu jana, lakini kwa kuwa jana tulikuwa mahakamani kwenye kesi yake nyingine ndiyo maana hakuweza kwenda kwani hakujua ingeisha muda gani,” alisema Kibatala.

Aliongeza “Kwahiyo leo alhamisi amekwenda central na mahojiano yameanza na sasa yuko na wakili Kiwhelu. Ameitwa kuhojiwa kuhusu mkutano wake na waandishi wa habari alipozungumzia suala la Ben Saanane “.

Chanzo:Bongo5.com

Advertisements