Papa Francis Kutafuta suluhu ya Mgogoro wa kisiasa Nchini Venezuela.

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amechukua hatua isiyotarajiwa na kuingilia kati kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa nchini Venezuela.Pope Francis shakes hands with Venezuela's President Nicolas Maduro during a meeting at the VaticanRais wa Venezuela Bw. Nicolas Maduro kushoto akikaribishwa na Papa Francis  

Wakati wa mkutano wa faragha na Rais Nicolas Maduro uliofanyika Vatican, Papa Francis ameomba kuongoza mashauriano kati ya rais huyo na viongozi wa upinzani ili kutafuta suluhisho la Mzozo huo.

Mjumbe wa Papa nchini Venezuela Emil Paul Tscherrig amesema pande zote mbili zimeahidi kufanya mashauriano rasmi Jumapili ijayo katika kisiwa cha Margarita, nchini Venezuela.

Lakini kupitia taarifa iliyopeperushwa mtandaoni, kiongozi wa upinzani Henrique Capriles amesema hakuna mazungumzo yoyote yaliyoanza na kwamba tangazo la kuanza upya kwa mashauriano ni njama ya serikali.

Wasiwasi umekuwa ukitanda Venezuela kutokana na kuahirishwa kwa kampeni za kura ya maoni ya kuamua kuhusu kuondolewa madarakani kwa Bw. Maduro.

Taifa la Venezuela mbali ya kukabiliwa na migogoro ya kisiasa pia linakabiliwa na matatizo ya kiuchumi Tangia aingie madarakani Rais Nicolas Maduro.

                                                 CHANZO:BBC SWAHILI

Nakualika ku like ukurasa wangu wa FB kwa kubofya hapa Facebook Au nifuate kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram na Twitter

Leave a comment